All jobs

DEREVA WA MALORI MAKUBWA

Abantu Tanzania

Job description

Majukumu Makuu 1. Kuendesha Safari za Masafa Marefu • Kuendesha malori ya HOWO na FAW kwa usalama kwenye safari za kimataifa, hasa Tanzania kwenda DRC. 2. Kutunza Mizigo • Kuhakikisha mizigo inapakiwa vizuri, inasafirishwa kwa usalama, na inafikishwa bila kuharibika au kupotea. 3. Taratibu za Mipakani • Kusimamia vibali vyote vinavyohitajika na nyaraka za forodha wakati wa kuvuka mipaka. 4. Ukaguzi na Matengenezo ya Gari • Kufanya ukaguzi wa gari kila siku kabla ya safari. • Kubaini na kutatua hitilafu ndogo za kawaida ili kuhakikisha gari linaendelea kuwa katika hali nzuri. 5. Kuzingatia Sheria • Kufuata sheria za usalama barabarani, viwango vya mwendo vinavyoruhusiwa, na taratibu za kampuni kuhusu mapumziko na matumizi ya mafuta. Sifa na Nyaraka Zinazohitajika • Leseni halali ya udereva daraja E. • Cheti cha mafunzo ya HGV (Heavy Goods Vehicle), PSV (Public Service Vehicle) au GDP (Good Driving Practice). • Kitambulisho cha Taifa (NIDA) halali. • Pasipoti halali ya kusafiria. • Namba ya TIN na usajili wa NSSF. • Cheti cha Tabia Njema (Police Clearance) cha hivi karibuni. • Cheti cha Uhakiki wa Leseni ya Udereva (Driving License Verification Certificate). Sifa Binafsi • Uzoefu wa kuendesha safari za masafa marefu na kuvuka mipaka. Uzoefu wa njia ya DRC ni faida ya ziada. • Uelewa mzuri wa mifumo ya malori, hasa HOWO na FAW. • Uaminifu, uvumilivu, na uwezo wa kufanya kazi kwenye safari ndefu.